Lugha Ya Kiswahili Na Dini.
Kiswahili ni nguzo muhimu sana katika jumuiya ya afrika mashariki na dunia nzima kwa jumla. Katika nchi ya Kenya kwa mfano, Kiswahili kimetumika pakubwa katika nyanja tofauti kama vile: siasa, utangamano, elimu, dini na biashara. Hizi tanzu zote ni muhimu katika nchi ambazo hutumia Kiswahili kama lugha mojawapo kuu katika mazungumzo. Kati ya nchi hizo, Kenya ni mojawapo, zingine ni Tanzania, Uganda na Rwanda kati ya nyinginezo ambazo zimeanza kukilaki Kiswahili katika mipaka yao.
Dini kwa nchia ya urahisi ni ule utambulizi na kanisa fulani ambalo linaabudu mungu ama miungu yao. Ukiristo ni dini ambayo hujitambulisha na uabudu wa mungu muumbaji wa nchi na mbingu. Wakiristo uamini kwamba mungu muumba alimtuma mwana wake yesu kristo kuukomboa ulimwengu kutoka janga la dhambi. Katika afrika mashariki ambao ndio wazungumzaji wakubwa wa Kiswahili, ukiristo umejigawanya kwa makundi mawili makuu. Kundi la kwanza ni lile la wanaoabudu siku ya kwanza ya juma; Jumaapili na lile linaloabudu siku ya saba/mwisho wa juma; Jumamosi. Lile kundi la Jumaapili lina wafuasi wengi wa Kikatoliki ambalo lina mizizi yake toka Roma huku lile la Jumamosi likiwa na wafuasi wa kiaedventista ambalo lina mizizi yake katika unabii wa mungu wa Biblia.
Nchi ya Tanzania na Kenya ambazo ni nchi zinakitumia Kiswahili kama lugha ya taifa zina wazungumzaji wengi wa Kiswahili. Takribani asilimia mia ya Watanzania ni wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili huku takribani asilimia sabini ya wakenya wakiwa wazungumzaji asili wa Kiswahili. Wamisenari wa kwanza walipofika katika bahari Hindi,watu wa pwani ya Kenya na Tanzania walikuwa wazungumzaji wa Kiswahili. Katika kuangazia vile wangefanya dini izambae kote Afrika mashariki,wakasambaza ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kule vijijini katika hali ya kuwasaidia hata wakongwe waweze kusoma biblia.
Ingawa lugha ya Kiingereza imetiliwa mkazo katika uzungumzaji himaya ya Afrika mashariki haswa nchi ya Kenya, lugha ya Kiswahili ndio inatumika kwa kiasi kikubwa katika uzungumzaji makanisani. Kuna makanisa mengi nchini Kenya, Tanzania, Uganda na hata Rwanda ambayo hukitumia Kiswahili kama lugha ya kwanza makanisani kama nchia moja ya kuhakikisha kwamba neno la mungu linawafikia watu wote kama anavyotuamuru Kristo kitabu cha Mathayo 28:19-20.
Ijapokuwa dini ya kikiristo ndio kubwa zaidi Afrika Mashariki, kuna dini zingine kama vile Hindu, Uislamu na pia kuna wale ambao hawaamini katika dini yoyote. Uislamu kwa mfano hukitumia Kiswahili katika mazungumzo na mahubiri kwa kiasi kikubwa sana. Katika kuwafunza wafuasi wageni pia ambao hawafahamu Hindu kama lugha yao, waamini wa kihindi huweza kusukumwa kukitumia Kiswahili kuwaelezea kuhusiana na dini hiyo. Ukiwa mgeni nchini Kenya kwa mfano na ukawa unatembea katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ama jiji kuu la Nairobi, utapiwa na mbumbuazi ukiwakuta wahindi na watu wa asili ya kichina wakikizungumza kwa urahisi Kiswahili ingawa labda si wazungumzaji fasaha. Hivyo ndivyo kilivyo Kiswahili kwa mwananchi wa Afrika Mashariki.
Lugha ya Kiswahili imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na lugha geni ya sheng’ haswa katika mazungumzo. Ingawa huo ndio uhalisia wa mambo, lugha ya sheng’ haijaathiri kwa ukubwa uzungumzaji wa Kiswahili katika mazingira ya dini. Dini ni muhimu sana katika maisha ya binadamu na ndio maana watu wengi hawachezi na kuchanganya lugha ya sheng’ katika uabudiaji wao. Yalivyo mahusiano ya watu kati ya wao kwa wao, ndivyo ilivyo dini kwa wafuasi hao kwani ni muhimu sana kwao katika ukombozi na kule kupata uzima wa milele. Kiswahili ni muhimu katika dini kama kilivyo kwa utangamano wa taifa na kinatumika kwa ukubwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki.