KISWAHILI NI MUHIMU KAMA CHOMBO CHA UTANGAMANO KWA WAKENYA.
Lugha ni mojawapo ya tanzu muhimu ya kuleta uwiano na utangamano katika jamii yoyote humu duniani. Kwa mfano, mkiristo ana lugha ya ukiristo ya kujitambuliza nayo kwa wakiristo wengine kama ilivyo lugha ya walio wafuasi wa mpira wa kandanda ama lugha wanayojitambulisha nayo vijana. Umuhimu wa lugha unaenda zaidi ya kujitambulisha hata ikawa mojawapo ya tanzu muhimu za kufanikisha uwepo wetu kama wanadamu na hata wanyama. Kuzungumza utumia lugha, kuimba ni kupasha ujumbe kutumia lugha, pia kuonya na hata kutoa maagizo.
Mwalimu Nyerere akiwa mmoja wa viongozi ambao nawadhamini sana katika Africa yote alikuwa mmojawapo wa watu ambao walikiangazia Kiswahili kwa umaakini sana kama chombo cha utangamano katika jumuia ya Africa mashariki. Mimi na wewe ni mashahidi wa jinsi ambavyo Kiswahili kimeisaidia Tanzania kuafikia malengo yao kwa njia ya utangamano, uwiano na kufukuza ukabila. Katika hotuba yake mwaka wa elfu moja mia tisa tisini na tano, mwalimu alitoa mfano wa Kenya na Uganda kama nchi mbili ambazo zilikuwa na ukabila mwingi sana. Angeamka leo, angepigwa na mshangao mkubwa jinsi ukabila na rushwa ulivyostawi kwa kina kirefu haswa nchini Kenya. Nchi ya Kenya na Tanzania ndizo nchi mbili katika himaya ya Africa ambazo zinakitumia kwa ukubwa Kiswahili. Lakini jambo moja ni kinzani, kwamba Tanzania ina utangamano mwingi kuliko Kenya. Kwa nini iwe hivyo? Kwa sababu hatujakidhamiria Kiswahili kama kipengee muhimu katika kutusaidia kuleta utangamano nchini.
Kiswahili kingetumika inavyopaswa, hatungekuwa na visa vingi vya utoaji rushwa, ukabila ungekuwa kitu ambacho kimesaulika na bila shaka uchumi wetu ungekuwa wa kupigiwa mfano. Kule kuitangulisha lugha yetu ya kwanza katika maongezi yetu hata katika mahali pasipostahili ni kama kumuulizia mtu mwingine kwamba unatoka kabila gani huku Kenya. Ina umuhimu wani kumuulizia mtu kuhusu kabila lake? Kwamba hata kama huna yanayohitajika katika kupata kazi fulani, utapewa tu juu wewe ni wa kabila fulani, upumbavu mkubwa huo. Ukabila na utoaji rushwa ni mambo mawili ambayo hayawezi kuachana kamwe. Kupigana vita na moja kati ya haya masaibu mawili ni kama kutenganisha wawili wanopendana; ni ngumu sana. Ni bayana kwamba tukikichukulia Kiswahili kwa umaakini tutaweza kuongeza utanagamano kati yetu na tunaweza kuwa watu wamoja; wakenya.
Kutenganiza kila kitu kwa njia ya ukabila na dini ni jambo moja mbaya sana. Vyama kutengenezwa kwa misingi ya kikabila ni kufanya vigumu urahisishaji wa kukipenyesha Kiswahili katikati ya nchi ambayo iekidharilisha sana Kiswahili kama nguso muhimu katika mikakati yake ya kukuza utangamano na uchumi. Lakini kuna uwezekano wa kuafikia malengo yetu kama nchi iwapo tutakichukulia Kiswahili kwa umuhimu mkubwa na kukitunza ili kiwe mojawapo ya vile vitu tunavyovidhaminia sana. Ukabila na vita vya kikabila, utoaji rushwa utapungushwa kwa ukubwa iwapo tutakuwa taifa moja la wakenya linalounganishwa na lugha moja; kiswahili. Hivyo ndivyo Kiswahili likivyo na umuhimu katika kuimakiza utangamano uwiano na hata ukuzaji wa kiuchumi.
Mwisho.